Ufaransa yaitandika Brazil, Sweden watinga hatua ya mtoano
29 Julai 2023![Timu ya Ufaransa](https://static.dw.com/image/66256625_800.webp)
Michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake inayoendelea huko New Zealand na Australia, Ufaransa wamewachapa mabingwa wa Amerika ya Kusini timu ya Brazil kwa mabao 2-1.
Nahodha wa Ufaransa Wendy Renard alifunga bao la pili na la ushindi mnamo dakika ya 83 ya mchezo. Matokeo hayo yameiweka Ufaransa katika uongozi wa kundi F ikiwa na pointi 4. Katika Mechi nyingine ya kundi hilo Jamaica wamemaliza dakika 90 na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Panama.Nigeria yaibabua Australia Kombe la DuniaNigeria yaibabua Australia Kombe la Dunia
Katika mchezo wa awali, Sweden walishinda bao 3-0 ndani ya dakika 7 kabla ya muda wa mapumziko wa kipindi cha kwanza dhidi ya Italia. Matokeo ya mwisho yalikuwa mabao 5-0 na kuipeleka moja kwa moja Sweden katika hatua ya mtoano ya Kombe la Wanawake.