1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yalitambua rasmi taifa huru la Palestina

23 Septemba 2025

Viongozi wa ulimwengu wamekusanyika mjini New York, Marekani kuhudhuria mkutano maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaolenga kuzifufua juhudi za kuundwa kwa mataifa mawili.

New York, Marekani 2025 | Bendera ya Umoja wa Mataifa
Umoja wa Mataifa: Taifa huru la Palestina ni "haki na sio zawadi." Picha: Spencer Platt/Getty Images

Akizungumza Jumatatu mwanzoni mwa mkutano huo, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ametangaza kuwa nchi yake sasa inalitambua rasmi taifa huru la Palestina.

Macron amesema lazima wafungue njia kwa ajili ya amani, na kuhakikisha kuna uwezekano wa suluhisho la mataifa mawili, ambapo Israel na Palestina zitaishi pamoja kwa amani na usalama.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan Al Saud, ameupongeza uamuzi huo wa Rais Macron akisema ni wa kihistoria, na kuzitaka nchi nyingine kuchukua hatua kama hiyo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema taifa huru la Palestina ni "haki na sio zawadi."

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Annalena Baerbock ametoa wito wa kuanzishwa kwa taifa "huru na lenye uwezo" la Palestina.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW