Ufaransa yapinga kuwa imeitelekeza Mali
28 Septemba 2021Matangazo
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Anne-Claire Legendre amesema mabadiliko ya kijeshi katika eneo la Sahel hayamaanishi kuwa Ufaransa inajitenga na Mali na wala sio uamuzi wa upande mmoja.
Ameongeza kwamba ni hatua iliyochukuliwa baada ya mashauriano na mamlaka ya Sahel pamoja na Mali.
Ufaransa imeyasema hayo baada ya Waziri Mkuu wa Mali Choguel Kokalla Maiga kuishutumu Ufaransa kuitelekeza nchi hiyo iliyokumbwa na mizozo kutokana na uamuzi wake wa kupunguza idadi ya wanajeshi mwaka huu.
Legendre amesisitiza kwamba Ufaransa itaendelea kushirikiana na Mali na mataifa mengine ya kundi la G5, kupambana na ugaidi ambao bado ni kipaumbele kwao.