1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yataka lipelekwe haraka Kikosi cha

17 Januari 2004

NEW YORK:
Waziri wa Mambo ya Ulinzi wa Ufaransa Bibi
Michèle Alliot-Marie ametoa mwito wa
kupelekwa haraka Kikosi cha UM cha kuhifadhi
amani nchini Ivory Coast. Kwa sababu hiyo
Ufaransa imelipa Baraza la Usalama la UM
mswada wa azimio kuhusu kikosi hicho, alisema
Waziri huyo baada ya kukutana mjini New York
na Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan. Lazima
juhudi za amani zisisitizwe kwa kuchukuliwa
hatua za kuyapokonya silaha makundi
yanayohasimiana katika nchi hiyo yenye vita
vya ndani, alisema Bibi Alliot-Marie. Kwa
sababu hiyo ni muhimu sana kipelekwe kikosi
cha amani cha UM, alisisitiza. Nayo Marekani
imesema ina shaka zake kuhusu kiwango kikubwa
cha wanajeshi 6,200 wa UM nchini Ivory Coast.