Ufaransa kuisadia Sudan kulipa deni la nje
17 Mei 2021Waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire amesema hayo leo kwenye ufunguzi wa mkutano wa kimataifa unaolenga kulisaidia taifa hilo lililopo kwenye mchakato wa kujitoa kwenye utawala wa kiimla hadi wa kidemokrasia.
Waziri huyo wa fedha amesema rais Emmanuel Macron atathibitisha hatua hiyo baadae leo. Waziri mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok anahudhuria mkutano huo unaofanyika mjini Paris, akisaka uungwaji mkono wakati taifa hilo likipambana kulipa deni la nje linalofikia dola bilioni 60 lakini pia akitaraji kupata makubaliano ya uwekezaji.
Soma Zaidi:Sudan:Mwaka mmoja baada ya kutimuliwa Bashir
Hamdok anashinikiza ujenzi mpya na kuleta mabadiliko kwenye uchumi uliozorota, lakini pia kuhitimisha hatua ya kutengwa kwa taifa hilo iliyochukuliwa katika enzi ya utawala wa Omar al-Bashir ambaye chini ya utawala wake wa miongo mitatu taifa hilo liligubikwa na hali ngumu na vikwazo vya kiuchumi.
Hamdok aliliambia shirika la habari la AFP kabla ya mkutano huo kuwa anaamini kwamba Sudan inaweza kukabiliana na deni hilo la nje iwapo litafanikiwa kuingia mikataba ya uwekezaji na nafuu ya madeni.
Waziri huyo wa fedha wa Ufaransa amesisitiza kwamba si suala la muda mfupi la kujenga upya uchumi utakaovutia na endelevu na kuongeza kuwa kwenye mkutano huo wana imani ya kuwashawishi wawekezaji binafsi kwamba kuna fursa muhimu za kibiashara nchini Sudan.
Kesho Jumanne, rais Macron atahudhuria mkutano wa kilele unaozungumzia masuala ya kiuchumi barani huko akiungana na Hamdok na viongozi wengine wa Afrika. Kwenye mkutano huo wakuu hao watajadiliana masuala kadhaa yenye leo la kukabiliana na upungufu wa fedha unaokaribia dola bilioni 300, uliosababishwa na janga la virusi vya corona.
Mkutano huo unaowakutanisha wakuu wengi wa Afrika utakuwa miongoni mwa mikutano mikubwa zaidi inayowakutanisha viongozi wengi wa ngazi za juu kwenye mikutano inayofanyika wakati wa janga la COVID-19. Lakini pia ni jukwaa litakalompa fursa rais Macron kujitanabahisha kwamba ushawishi wake unavuka mipaka ya mataifa yanayozungumza Kifaransa.
Kusanyiko hilo pia litashuhudia uwepo wa rais Paul Kagame wa Rwanda, katika wakati ambapo Paris inashinikiza maridhiano na Kigali baada ya ripoti ya kihistoria kuweka wazi kwamba Ufaransa ilishindwa kuyazuia mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Sudan iliondolewa kwenye orodha mbaya ya Marekani kama mmoja ya wafadhili wa ugaidi mnamo mwezi Disemba na kuondolewa vikwazo vikubwa vya uwekezaji wa kigeni, lakini hata hivyo bado linakabiliwa na changamoto kubwa.
Serikali yake imekuwa ikishinikza kufikia makubaliano ya amani na makundi ya waasi ili kumaliza mzozo katika jimbo la Vita vya kikabila huko Darfur vyazusha hofu kubwaDarfur liliko magharibi mwa nchi hiyo pamoja na majimbo ya kusini ya Kordofan na Blue Nile.
Mashirika: AFPE