1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfilipino

Ufilipino: Gavana na watu wengine 5 wauawa kwa risasi

4 Machi 2023

Gavana wa jimbo la katikati mwa Ufilipino pamoja na watu wengine watano wameuawa leo kwa kufyatuliwa risasi na watu wasiojulikana.

Philippinen | Polizeiauto verlässt Einsatzort
Picha: Mark R. Cristino/dpa/picture alliance

Hili ni shambulio la hivi punde dhidi ya maafisa wa serikali. Roel Degamo, 56,  alikuwa gavana wa jimbo la Negros Oriental.

Polisi wamesema washukiwa sita waliokuwa wamebeba bunduki na waliovalia sare zinazofanana na zile zinazovaliwa na wanajeshi,  waliingia katika nyumba ya gavana huyo aliyekuwa akitoa msaada kwa wananchi katika mji wa Pamplona na kuanza kufyatua risasi.

Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos JrPicha: Sean Kilpatrick/empics/picture alliance

Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos amelaani kile alichokitaja kuwa ni "mauaji" ya mshirika wake wa kisiasa na kuahidi kuwafikisha wahusika wa uhalifu huo mbele ya vyombo vya sheria. Takriban wanasiasa watatu wameuawa kwa risasi tangu uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW