1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfilipino

Ufilipino na washirika wake wafanya luteka Bahari ya China

Saleh Mwanamilongo
28 Septemba 2024

Wanajeshi wa Ufilipino, Australia, Japan, New Zealand na Marekani wamefanya luteka za pamoja baharini katika eneo la kipekee la kiuchumi la Ufilipino.

Ufilipino, Japan, New Zealand na Marekani zafanya luteka za pamoja za baharini
Ufilipino, Japan, New Zealand na Marekani zafanya luteka za pamoja za bahariniPicha: Daniel Ceng Shou-Yi/ZUMA/picture alliance

Mkuu wa majeshi ya Ufilipino Jenerali Romeo Brawner amesema luteka hizo zimefayika katika Bahari ya China Kusini na zinalenga kuimarisha ushiriano wa kimkakati baina ya nchi hizo.

Brawner amesema New Zealand ilijiunga na shughuli hizo kwa mara ya kwanza, na kuongeza mwelekeo mpya wa juhudi za ushirikiano.

Ufilipino imekuwa ikiongeza ushirikiano wa mafunzo na kuboresha uhusiano wa ulinzi na washirika wake dhidi ya China. Kwa upande wake, meli na ndege za China zilifanya doria hii leo kwenye eneo la Scarborough Shoal katika Bahari ya Kusini ya China.