1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufilipino kushirikiana na ICC katika waranti ya Duterte

Sylvia Mwehozi
14 Novemba 2024

Serikali ya Ufilipino imesema vyombo vyake vya kiusalama havitosita kutoa ushirikiano ikiwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, itataka kukamatwa kwa Rais wa zamani Rodrigo Duterte.

Rodrigo Duterte(kulia)
Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte(kulia)Picha: Bullit Marquez/AP Photo/picture alliance

Serikali ya Ufilipino imesema vyombo vyake vya kiusalama havitosita kutoa ushirikiano ikiwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, itataka kukamatwa kwa Rais wa zamani Rodrigo Duterte. Hayo ni kufuatia uchunguzi unaoendelea juu ya vifo vilivyotokea wakati wa kampeni ya Durtete dhidi ya wauza mihadarati wakati alipokuwa mamlakani.

Mahakama ya ICC imekuwa ikichunguza mauaji yaliyoenea wakati Duterte alipokuwa meya wa  mji wa kusini mwa nchi wa Davao na baadaye kama rais kutoka mwaka 2016 hadi 2020.

Wakati wa kikao cha bunge siku ya Jumatano kuhusu kampeni hiyo, Duterte alisema hana hofu na ICC na kuitaka iharakishe katika uchunguzi wake.Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte atetea vita dawa za kulevya

Mashirika ya haki za binadamu yanakadiria kwamba zaidi ya watu 20,000 waliuawa wakati wa kampeni hiyo iliyoamriwa na Durtete.