1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUfilipino

Ufilipino yaishtumu China kuwa "mvurugaji mkubwa" wa amani

27 Agosti 2024

Waziri wa ulinzi wa Ufilipino Gilberto Teodoro ameishtumu China kwa kuitaja nchi hiyo kuwa mvurugaji mkubwa zaidi wa amani katika Bahari ya kusini mwa China.

Bendera ya Ufilipino inapepea kutoka kwa meli iliyochakaa ya Jeshi la Wanamaji la Ufilipino ambayo imekwama tangu 1999 katika Bahari ya Kusini ya China.
Bendera ya Ufilipino inapepea kutoka kwa meli iliyochakaa ya Jeshi la Wanamaji la Ufilipino ambayo imekwama tangu 1999 katika Bahari ya Kusini ya China.Picha: Erik De Castro/REUTERS

Waziri Gilberto Teodoro ametoa mwito kwa nchi washirika kuishinikiza China kusitisha kile walichokiita "shughuli zake haramu” katika Bahari ya kusini mwa China.

Ameuambia mkutano wa kila mwaka wa kijeshi wa kanda ya Indo Pasifiki kwamba Ufilipino ina nia ya dhati ya kulinda uhuru wake.

Soma pia: Mzozo wa Bahari ya China Kusini watishia biashara ya kimataifa

Brunei, Malaysia, Taiwan na Vietnam zinadai kumiliki sehemu tofauti za Bahari ya kusini mwa China, moja kati ya njia kuu za biashara na usafiri wa meli yenye thamani ya zaidi ya dola trilioni 3 kila mwaka.

China inapinga uamuzi wa mwaka 2016 wa mahakama ya kudumu ya usuluhishi iliyoko mjini The Hague ulioonyesha kuwa madai ya Beijing kuhusu Bahari ya kusini mwa China hayana msingi chini ya sheria za kimataifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW