1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufilipino yakosoa mazoezi ya kijeshi ya China Taiwan

31 Desemba 2025

Wizara ya ulinzi ya Ufilipino imesema ina wasiwasi kuhusu mazoezi ya kijeshi ya China karibu na kisiwa cha Taiwan kinachojitawala chenyewe. Ufilipino imesema mazoezi hayo yanatishia amani na uthabiti wa kikanda.

Philippinen Manila | Gilberto Teodoro
Waziri wa ulinzi wa Ufilipino Gilberto Teodoro Picha: Basilio Sepe/AP Photo/picture alliance

Waziri wake Gilberto Teodoro amesema hali inayoshuhudiwa inaendelea "kutanua ufa" katika eneo ambalo tayari ni tete na athari zake zinaweza kutanuka zaidi na kulemaza yaliyopwaya, miongoni mataifa jirani na mlango bahari wa Taiwan na kanda nzima ya bahari ya Hindi na Pasifiki.

China kwa upande wake imepuzilia mbali nchi yoyote inayokosoa mazoezi yake ya kijeshi ikiwemo Japan, Australia na baadhi ya nchi za Ulaya ikisema ukosoaji huo "hauna msing".

China ilianzisha mazoezi hayo ya kijeshi siku ya Jumatatu yanayojumuisha meli za kivita, wapiganaji, makombora na madroni. Mazoezi hayo yanalenga kuonesha utayari wa kukabiliana kupitia majini, kukizingira kisiwa hicho hasa katika bandari na maeneo yake muhimu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW