1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Ufilipino yawakamata raia wake wanaoifanyia ujasusi China

4 Machi 2026

Serikali ya Ufilipino imesema imewakamata baadhi ya raia wake kwa kuwashuku kuwa wanaifanyia kazi ya upelelezi China, kuhusiana na "suala muhimu la usalama wa taifa."

Polisi wa Ufilipino wakiwa kazini
Polisi wa Ufilipino wakiwa kaziniPicha: Ted Aljibe/AFP

Ufilipino inasema hatua hiyo inaonesha wazi haja ya uwepo wa sheria kali dhidi ya upelelezi na mataifa ya kigeni kuingilia masuala ya nchi hiyo.

Mamlaka hazikutoa taarifa kuhusiana na kisa hicho, ikiwemo ni watu wangapi wlaiokamatwa au iwapo wamefunguliwa mashtaka.

"Shughuli za watu hawa wanaozifanyia shirika la ujasusila China zimesitishwa," imesema taarifa ya Baraza la Usalama la Kitaifa la Ufilipino.

"Hatua stahiki dhidi ya wahusika ambao wote ni raia wa Ufilipino, zimechukuliwa. Wote wamekiri kuifanyia China ujasusi na wanashirikiana na mamlaka," iliongeza taarifa hiyo.

Walinzi wa pwani ya China wakiwaokoa mabaharia wa Ufilipino katika Bahari ya Kusini mwa ChinaPicha: China Coast Guard/Xinhua/picture alliance

Uhusiano kati ya China na ufilipino umezidi kuwa mbaya kutokana na makabiliano ya mara kwa mara katika Bahari ya Kusini mwa China, huku pande zote mbili zikizidisha vita vyao vya maneno ambavyo vimejitokeza pia katika miotandao ya kijamii.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW