1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UfisadiUganda

Uganda yapoteza takriban dola bilioni 2.5 kwa ufisadi

7 Oktoba 2024

Uganda inapoteza takriban dola bilioni 2.5 kutokana na ufisadi kila mwaka, sawa na karibu robo ya bajeti yake ya mwaka.

Uganda | Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekuwa akiahidi kushughulikia changamoto ya rushwa, lakini hilo halijafanikiwa Picha: SIMON MAINA/AFP/Getty Images

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Mkuu wa Ofisi inayopambana na ufisadi alipozungumza na shirika la habari la AFP mapema hii leo.

Ufisadi ni tatizo kubwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki, ambalo linashika nafasi ya 141 kati ya 180 katika ripoti ya kimataifa ya nchi zenye kiwango cha juu cha ufisadi duniani.

Hivi karibuni yaliibuka maandamano nchini Uganda ya kupinga ufisadi na Rais Yoweri Museveni amekuwa akiahidi mara kwa mara kwamba atafanyia kazi kashfa hizo zinazowakabili maafisa wa umma.

Ripoti hiyo inatolewa wiki moja baada ya Museveni kumsamehe afisa mmoja wa serikali aliyetumikia miaka mitano ya kifungo cha miaka 10 jela baada ya kuiba dola milioni 1.2 kwenye hazina ya serikali, suala lililoibua hasira kutoka kwa mashirika ya kiraia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW