1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroNiger

UN: Ugaidi na uhalifu wa kupangwa vyaongeza kitisho Sahel

13 Julai 2024

Umoja wa Mataifa umesema ugaidi na uhalifu wa kupangwa na vurugu makundi ya itikadi kali ni "kitisho kinachosambaa" katika hilo eneo tete la Afrika hadi pwani ya Afrika Magharibi.

Leonardo Santos Simao
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Sahel na Afrika Magharibi, Leonardo Santos Simao aonya dhidi ya kuenea kwa itikadi kaliPicha: Elisabeth Asen/DW

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya eneo la Sahel Leonardo Simao amesema ugaidi na uhalifu wa kupangwa na vurugu makundi ya itikadi kali yenye mafungamano na al-Qaida na kundi linalojiita Dola la kiislamu, ni "kitisho kinachosambaa" katika hilo eneo tete la Afrika hadi pwani ya Afrika Magharibi.

Mjumbe huyo anayesimamia na Afrika Magharibi amesema jana Ijumaa kwamba umakini katika kupambana na ugaidi umekua na matokeo madogo katika kukomesha biashara haramu iliyokithiri katika eneo la Sahel na juhudi hizo zinahitaji polisi zaidi.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Katibu Mkuu Antonio Guterres kuhusu Sahel na Afrika Magharibi, mamia ya watu wameuawa katika eneo hilo katika nusu ya kwanza ya 2024, katika mashambulizi ya kigaidi, wengi wao wakiwa ni raia.

Watu wengi walikufa Burkina Faso, Mali na Niger, ambako wakuu wake wa kijeshi mwezi Machi walitangaza kuunda kikosi cha pamoja cha usalama kupambana na ugaidi, ingawa bado hakijaanza kazi.

Nchi hizo tatu zinazidi kukata Harakati za kijeshi za Marekani hatarini eneo la Saheluhusiano na jeshi la Marekani na kushirikiana na Urusi kukabiliana na changamoto zake za usalama.

Wakuu wa nchi za Mali Assimi Goita, Abdourahamane Tiani wa Niger na Ibrahim Traore wa Burkina Faso wakati wa mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi na serikali wa Muungano wa Nchi za Sahel (AES) huko Niamey, Niger Julai 6, 2024.Picha: Mahamadou Hamidou/REUTERS

Simão hata hivyo hakuzungumzia ushirikiano huo wa kimataifa wa nchi hizo, lakini alisema kujitoa kwao kwenye Ushirikiano wa Uchumi wa Afrika Magharibi, ECOWAS "utakuwa na madhara kwa pande zote mbili." Hata hivyo aliipongeza ECOWAS kwa kuchukua' "mkondo thabiti" wa kujadiliana na Burkina Faso, Mali na Niger na kuzitaka nchi hizo kudumisha umoja wa kikanda.

Guterres: "ukosefu wa usalama unaendelea kuathiri haki za binadamu"

Mjumbe huyo aidha, alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuendelea kuunga mkono Mpango wa Accra, jukwaa la kijeshi linaloijumuisha Burkina Faso na nchi jirani ili kuzuia kuenea kwa itikadi kali katika eneo la Sahel.

Takwimu za Taasisi ya inayofuatilia migogoro ya Silaha, ya Armed Conflict Location and Event Data Project, zimeonyesha kulikuwa na vifo 361 vinavyohusiana na migogoro nchini Niger miezi mitatu ya kwanza ya 2024.

Kulingana na Guterres, ukosefu wa usalama wa kikanda "unaendelea kuathiri vibaya hali ya kibinadamu na haki za binadamu."

Ripoti zimesema watu milioni 25.8 nchini Burkina Faso, Mali, Niger na Nigeria wanahitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu.

Nchi hizo nne zilikuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani milioni 6.2 na wakimbizi 630,000 hadi mwezi Aprili. Aidha, watu milioni 32.9 walikabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula.

Soma pia. Mali, Niger, Burkina Faso wanakabiliwa na uasi wa jihadi kwa muda mrefu