1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda, DRC wafanya mashambulizi ya pamoja dhidi ya ADF

30 Novemba 2021

Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameanzisha operesheni ya pamoja ya mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la waasi la ADF linalofanya harakati zake mashariki mwa Kongo.

Afrika Uganda Edward Katumba Wamala
Picha: AFP via Getty Images

Msemaji wa jeshi la Uganda, amethibitisha asubuhi ya leo kufanyika kwa mashambulizi hayo.

Kupitia mtandao wa Twitter, msemaji huyo alisema kwamba kwa pamoja majeshi ya pande hizo mbili yalifanya operesheni ya angani na makombora kwenye kambi za ADF.

Mamlaka nchini Uganda zinalihusisha kundi la ADF na miripuko ya mwezi uliopita yaliyouwa watu kadhaa mjini Kampala.

Hapo jana, serikali ya Kongo ilikuwa imekataa kuwa ilikubaliana kufanya operesheni za pamoja na jeshi la Uganda dhidi ya kundi hilo, ingawa ilikubali kuwa pande hizo mbili zinashirikiana kwenye kupeana taarifa za kijasusi.

Mapambano hayo kati ya jeshi la Congo na makundi ya wanamgambo yameripotiwa katika vijiji vya Busumo, Rukobero na Mashuba ambapo jeshi limelenga ngome za waasi hao wanatuhumiwa kuungana na makundi ya Mai-Mai ili kuzorotesha usalama hususan katika bonde la mto Ruzizi. 
Bila kutoa taarifa zaidi, msemaji wa jeshi la FARDC kusini mwa mkoa wa Kivu kusini meja Dieudonné Kasereka amehakikisha kwamba juhudi zinafanyika ili kuwatokomeza waasi hao aliowaita wa kigeni na makundi mengine ya wanamgambo raia wa Congo wanaotatiza raia eneo hilo. 
Pamoja na kupongeza jeshi kwa juhudi hizo, baadhi ya asasi za kiraia katika mkoa wa kivu kusini zinaendelea kuuliza maswali juu ya kushindwa kupata suluhisho la kudumu dhidi ya makundi hayo yenye silaha. 

Operesheni ya pamoja ya DRC na Uganda yamaanisha nini?

This browser does not support the audio element.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa Jumatatu jioni, waziri wa habari Patrick Muyaya, ambaye pia ni msemaji wa serikali ya Congo, alisema "Hatujasema hapa kwamba watatusaidia, lakini tumesema kwamba kutakuwa na vitendo vya pamoja kwa sababu leo tishio linahitaji tufanye mashambulizi ya pamoja."

Muyaya aliffanua zaidi kwamba  kama serikali wanajua unyeti wa watu wao kuhusu masuala ya kikanda. "Na leo hii, kuhusiana na tishio linaloongezeka, majeshi yetu yanaangalia kile tunachokiita vitendo vilivyolengwa, kutokana na mienendo ya magaidi,”amesema Muyaya.