1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda imeanza kutowa chanjo ya homa ya manjano nchi nzima

29 Mei 2024

Uganda imeanzisha zoezi la nchi nzima la kutowa chanzo ya ugonjwa wa homa ya manjano hatua inayolenga kusaidia kuwalinda wakaazi wake dhidi ya ugonjwa huo unaosababishwa na mbu na ambao umekuwa kitisho kwa muda mrefu.

Homa ya manjano
Uganda imeanza kampeni ya kutowa chanjo ya homa ya manjano nchi nzimaPicha: Reuters/P. Whitaker

Dr Michael Baganizi afisa anayehusika na chanjo katika wizara ya afya ya nchi hiyo amesema dozi moja ya chanjo hiyo inatolewa bure kwa raia kati ya mwaka mmoja na miaka 60.

Kabla ya kampeini hiyo kuanzishwa Waganda walihitajika kupata chanjo hiyo ya homa ya manjano katika hospitali za binafsi.

Kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili,tayari nchi hiyo ilikuwa imeshatowa chanjo hiyo kwa watu milioni 12.2 kati ya milioni 14 iliyokuwa imewalenga kwenye kampeini yake hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW