1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda inaongoza mazungumzo ya amani Kongo

23 Julai 2024

Uganda inasimamia mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na muungano wa makundi ya waasi likiwemo kundi la M23.

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta ziarani Kongo
Kenya ilikuwa mpatanishi wa mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Benjamin Kasembe/DW

Afisa katika ofisi ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameliambia shirika la habari la AFP kuwa ujumbe wa ngazi ya juu kutoka serikali ya Kongo na muungano wa waasi unaofahamika kama M23/AFC wanakutana mjini Kampala kuleta amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Soma pia: Nyongeza ya muda wa kusitisha mapigano yaheshimiwa Kongo

AFC au Muungano wa Mto Kongo, ulitangazwa Desemba mwaka wa 2023 na Corneille Nangaa, aliyekuwa mkuu wa tume ya uchaguzi ya Kongo, na ambaye anaishi uhamishoni Kenya. Afisa huyo wa Uganda amesema Rais Museveni pia atashiriki katika mazungumzo hayo pamoja na aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ambaye amekuwa mpatanishi katika mzozo huo kwa niaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Huku mazungumzo hayo yakithibitishwa na chanzo ndani ya M23, Kinshasa imesema hakuna yeyote aliyepewa mamlaka na serikali kufanya mazungumzo yoyote na makundi ya kigaidi. Chanzo hicho kimesema mazungumzo hayo bado hayajaanza. Angola na Kenya zilishiriki katika mazungumzo ya upatinishi kati ya pande zinazohasimiana katika siku nyuma.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW