1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Uganda na DR Congo yaunda kamati kushughulikia mipaka

5 Septemba 2024

Kazi za Kamati ya Pamoja ya Kiufundi kati ya DRC na Uganda kwa ajili ya kuandaa bajeti ya kurekebisha mipaka ya pamoja kati ya nchi hizo mbili zimezinduliwa mjini Goma Jumatano, tarehe 04 Septemba, Mashariki mwa DRC.

Uganda Mpondwe | Kivuko kuingia Congo
Watu wakipita barabara inayoelekea mpaka wa Mpondwe kuingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka UgandaPicha: Ronald Kabuubi/AP Photo/picture alliance

Hii inafanywa kwa lengo la kutafuta njia na mbinu za kutatua mgogoro wa ardhi kwenye mpaka kati ya nchi hizi mbili.

Kazi ya urekebishaji wa mipaka ilifunguliwa na Gavana wa kijeshi wa Kivu ya Kaskazini, Meja Jenerali Peter Cirimwami, mbele ya ujumbe wa Uganda ukiongozwa na Kanali Naboth Mwesigwa.  

"Hakuna mgogoro ambao hauwezi kutatuliwa."

 Hii ndiyo fikra ambayo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda zitazingatia kwa siku tatu, kuanzia tarehe 4 hadi 6 Septemba, kujadili bajeti itakayowezesha kuweka alama ya mpaka wa pamoja ambao unaanzia Mlima Sabinyo katika DRC hadi Bwindi nchini Uganda, umbali wa kilomita 71. Hii ni fursa ya kijamii, kiuchumi, kihistoria, na kitamaduni, kwa sababu ni mwanzo wa kutatua mgogoro uliosababishwa na mpaka huu, kama alivyoeleza Gavana wa kijeshi wa Kivu ya Kaskazini, Meja Jenerali Peter Chirimwami: 

"Mpaka ni fursa ya kijamii, kihistoria, kiuchumi, na kitamaduni. Hata hivyo, pia umekuwa chanzo cha migogoro, mapambano, vita vya uvamizi, na upinzani wa kizalendo, kwa bahati mbaya, na athari nyingi na za aina mbalimbali kwenye hali za maisha ya watu." 

Uganda yakanusha shutma za kuiunga mkono M23

This browser does not support the audio element.

Soma pia: Uganda inaongoza mazungumzo ya amani kati ya pande zinazohasimiana Kongo

 Kiongozi wa ujumbe wa Uganda, Kanali Naboth Mwesigwa, alisema kuwa ana matumaini juu ya mafanikio ya mkutano huu licha ya kuchelewa kwake kutekelezwa. Alisema: "Tuko hapa kwa mkutano kati ya ujumbe wa Uganda na ujumbe wa DRC, unaohusu suala la kuweka alama ya mpaka kati ya Uganda na DRC. Uganda iko tayari na ina nia ya kuweka mipaka hiyo, kuchelewa kunatokana na ukweli kwamba taratibu za kuweka mipaka hiyo bado hazijawekwa. Siwezi kuita hili ucheleweshaji, hatucheleweshi, lakini kuna taratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa ili kuhakikisha kuna alama sahihi ya mpaka."

Soma pia: Jeshi la Uganda limemuuwa kamanda wa kundi la waasi nchini Congo

 Baada ya kazi hizi, ramani ya njia itaundwa kama hati itakayozifunga nchi hizi mbili katika mchakato wa kurekebisha mipaka yao ya pamoja.

Ni wataalamu wa Kamati ya Kudumu ya Mipaka kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ambao wanashiriki katika vikao hivi huko Goma. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW