Uganda na hofu ya kutokea vurugu Kenya
27 Februari 2013Pamoja na kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki, rais Museveni ndiye rais ambaye amekuwa madarakani kwa muda mrefu na kulingana na desturi za kiafrika, ushauri wa wazee huwa jambo muhimu sana.
Uganda usafirisha bidhaa zake nyingi kupitia mipaka ya Kenya kama vile Busia na Malaba na ikiwa kutakuwa na machafuko yoyote nchini Kenya, Uganda bila shaka uathirika. Machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 nchini Kenya yalisababisha upungufu wa mafuta ya gari na bidhaa muhimu ambazo zilikwama kwenye bandari ya Mombasa.
Ahadi ya kukabiliana na tatizo la mafuta
Uganda wakati huo haikuwa imeweka akiba ya mafuta jambo lililoathiri sana usafiri. Sasa Rais Museveni anawahakikishia wananchi wake kuwa hilo halitatokea tena. "Ule wakati lilikuwa jambo la kushangaza na hatukua tunatarajia machafuko kutokea Kenya na ndio sababu tukapatikana tukiwa hatujajitayarisha. Ingawa hatutarajii shida zozote nchini Kenya, sasa hivi tumejitayarisha na ndio sababu tukaifungua barabara ya kusini ya kusafirisha bidhaa kupitia nchini Tanzania. Tumejiandaa sasa". Alisema rais Museveni.
Wafanyi biashara wa Uganda upendelea kusafirisha bidhaa zao kupitia nchini Kenya kwa sababu hiyo ndio njia fupi ukilinganisha na ile ya Tanzania. Ingawa rais Museveni anawaakikishia wananchi wake kuwa kufunguliwa kwa barabara ya kupitia Tanzania kutahakikisha kuwa hawakosi bidhaa wanazohitaji, wananchi wanahofia kuwa bei ya bidhaa hizi huenda ikapanda kwa sababu ya bei ghali ya usafirishaji wa bidhaa hizi kupitia Tanzania.
Bei ya dola imezidi kupanda
Tayari, bei ya dola imepanda. Mojawapo ya sababu zinazochangia ikiwa wafanyibiashara wanaziitaji dola sana wanunue bidhaa za kutosha ili kuhakikisha kuwa hawataathirika na lolote lile litakalotokea nchini Uganda.
Bei ya dola ikipana, mafuta nayo yanapanda. Kuanzia wiki jana, bei ya lita moja ya petroli imepanda kutoka 3600 pesa za uganda na kufikia shilingi 3,900 ambazo ni sawa na dola moja na nusu pesa za marekani.
Mwandishi wetu wa Kampala Leylah Ndinda alihudhuria kikao cha waandishi habari kilichoitishwa na rais Yoweri Museveni nyumbani mwake Rwakitura magharibi mwa Uganda na kututumia ripoti ifuatayo. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya kusikilizia masikioni hapo chini.
Mwandishi Leyla Ndinda
Mhariri Josephat Charo