1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUganda

Uganda: Waliokufa maporomoko ya udongo wafikia 40

21 Desemba 2024

Mamlaka nchini Uganda zimesema leo kwamba idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maporomoko makubwa ya udongo yaliyotokea kiasi wiki tatu zilizopita imefikia 40.

Eneo layikotokea maporomoko ya udongo nchini Uganda.
Eneo layikotokea maporomoko ya udongo nchini Uganda.Picha: Nakasiita/AP Photo/picture alliance

Mwishoni mwa mwezi Novemba, zaidi ya nyumba 40 zilifukiwa na vifusi vya udongo baada ya kutokea maporomoko  yaliyosababishwa na mvua kubwa. Inahofiwa zaidi ya watu 100 walifukiwa wakiwa hai.

Mkuu wa Mkoa wa Bulambuli kulikotokea janga hilo, Faheera Mpalanyi, ameliambia shirika la habari la dpa kwamba hadi sasa juhudi za utafuataji watu zinaendelea lakini zinatatizwa na barabara pamoja na madaraja yaliyoharibiwa.

Amesema mamlaka nchini humo zinaamini hakuna manusura wanaoweza kupatikana. Mpalanyi amesema hivi sasa zaidi ya watu 2,500 walioathiriwa na janga hilo wanahifadhiwa kwenye kambi za muda za mahema.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW