Uganda watishia kuondoa wanajeshi wake wa kulinda amani
6 Novemba 2012Matangazo
Hayo yamesemwa baada ya ripoti ya umoja huo kuituhumu Uganda kuwa kinasaidia uasi huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Hivi sasa taifa hilo lina wanajeshi takribani 8,000 ikiwa ni pamoja na huko Somalia na katika jimbo la Darfur nchini Sudan. Kutoka kampala Sudi Mnette amezungumza na Msemaji wa Jeshi la Uganda, Kanali Felix Kulayigye na kwanza anaelezea kwanini wanatishia kujiondoa katika shughuli za kimataifa za kulinda amani?
(kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman