1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Uganda yaagiza kuzimwa kwa mtandao wa Intaneti

13 Januari 2026

Uganda imeagiza kuzimwa kwa mtandao wa intaneti siku mbili kabla ya uchaguzi, wakati Rais Yoweri Museveni akitafuta kuendeleza utawala wake wa takriban miaka 40.

Uganda Kampala 2026 | Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Picha za kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu nchini UgandaPicha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Tume ya Mawasiliano ya Uganda imetuma barua kwa kampuni za kutoa huduma za intaneti ikisema hatua hiyo inalenga kupunguza kusambaa kwa taarifa potofu mtandaoni na kuzuia uchochezi wa vurugu wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa yoyote kutoka serikalini kuhusu hatua hiyo ya kuzimwa kwa mtandao wa Intaneti. Maafisa walisema mamlaka hazikutaka "kumiliki" uamuzi huo.

Hii ni licha ya serikali kuahidi mara kadhaa kwamba intaneti haitazimwa wakati wa uchaguzi, ikisisitiza kupitia mtandao wa X tarehe 5 Januari kwamba madai ya kuzimwa kwa mtandao "si ya kweli na yanakusudia kuleta hofu kwa umma."

Uganda iliwahi kuzima intaneti wakati wa uchaguzi wa mwaka 2021, uchaguzi uliokumbwa na madai ya wizi wa kura na ukandamizaji wa upinzani unaoongozwa na mwanamuziki aliyegeuka mwanasiasa, Bobi Wine, ambaye anawania tena urais mwaka huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW