1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Uganda yajiandaa kuwazika wahanga wa shambulizi la ADF

18 Juni 2023

Ndugu na jamaa za wahanga wa shambulizi la waasi wa ADF jana Jumamosi huko nchini Uganda wanajiandaa kuwazika ndugu zao, huku kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis akiulaani vikali unyama huo.

Uganda | Angriff auf eine Schule in Uganda | Lhubiriha-Sekundarschule in Mpondwe
Picha: AP Photo/picture alliance

Ndugu na jamaa za wahanga wa shambulizi la waasi wa ADF jana Jumamosi huko nchini Uganda wanajiandaa kuwazika ndugu zao, huku kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis akiulaani vikali unyama huo.

Watu 42 waliuawa katika shambulizi hilo miongoni mwao wakiwa ni wanafunzi 38, na serikali ya Uganda sasa inaimarisha zaidi doria katika eneo mpaka wake na eneo tete la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako tukio hilo limetokea.

Meya wa kijiji cha Mpondwe, Selevest Mapoze amesema mmoja ya waliojeruhiwa jana amefariki usiku wa kuamkia leo na wakazi wengi wamekwenda kuchukua miili ya jamaa zao iliyohifadhiwa katika chumba cha maiti.

Papa Francis amesema anawaombea wanafunzi waliokumbwa na tukio hilo, huku katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres ambaye pia amelaani shambulizi hilo akisisitizia umuhimu wa juhudi za pamoja za kupambana na usalama duni kwenye mipaka kati ya Kongo na Uganda.