1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yakanusha madai ya kulisaidia kundi la M23

10 Julai 2024

Uganda leo imeyatupilia mbali madai yaliyotolewa na ripoti ya jopo la wataalamu la Umoja wa Mataifa kuwa nchi hiyo inawaunga mkono waasi M23 wanaopigana na majeshi ya serikali mashariki mwa Kongo.

Kongo | Wanajeshi huko Beni, DRC
Wanajeshi washiriki oparesheni ya pamoja ya jeshi la Uganda na DRC dhidi ya vikosi vya jeshi katika eneo la Beni, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Desemba. 8, 2021.Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Ripoti hiyo iliyoandaliwa kwa ombi la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imetaja kuwepo uungaji mkono wa idara za ujasusi za Uganda kwa kundi la M23. Alipoulizwa na waandishi hbaari mjini Kampala, Naibu Msemaji wa masuala ya ulinzi wa taifa Deo Akiiki amepuuza tuhuma hizo akizitaja kuwa "kichekesho, zisizo na msingi wala haziingii akilini".

Amesema vikosi vya Uganda vimekuwa vikifanya kazi bega kwa bega na wenzao wa Kongo kusaidia kurejesha utulivu mwashariki mwa Kongo. Akiiki amebainisha kuwa nchi hizo mbili zinashirikiana kutengeneza mazingira ya kuwepo amani jambo ambalo limesaidia kuimarisha mahusiano yao.

Mbali ya Uganda, ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa pia imeitaja Rwanda kuwa na dhima kubwa kwenye mzozo wa Kongo kuwasaidia waasi wa M23.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW