1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Uganda yapitisha muswada wa sheria ya mapenzi ya jinsia moja

2 Mei 2023

Bunge la Uganda limepitisha muswaada wa sheria ambao kwa sehemu kubwa haujafanyiwa marekebisho kuhusu watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Uganda | LGBTQ Gesetz
Picha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Licha ya mabadiliko kadhaa yaliyofanyika, muswaada huo mpya umebakisha vingi ya vipengele vinavyoruhusu hatua kali zaidi dhidi ya jamii hiyo, ikiwemo adhabu ya kifo kwa atakayekutwa na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja na kifungo cha miaka 20 kwa  kuhamasisha juu ya vitendo hivyo.

Soma Zaidi: Marekani yaahirisha mkutano wa VVU/UKIMWI nchini Uganda kufuatia sheria tata ya LGBTQ

Wanaharakati wanasema muswaada huo huenda ukazitazama harakati za kutetea haki za jamii hiyo ya LGBTQ kama kitendo cha kihalifu. Rais Yoweri Museveni mwezi uliopita aliurudisha muswaada huo bungeni na kuwaomba wabunge kufanyia marekebisho vipengele kadhaa vya muswaada wa mwanzo na kulegeza baadhi ya hatua.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW