1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yasaka ufadhili wa kuzalisha megawati 1,600 za umeme

2 Oktoba 2024

Uganda inasaka ufadhili wa ujenzi wa mitambo mitatu ya kuzalisha umeme wa nyongeza wa maji wa zaidi ya megawati 1,600, kwa lengo la kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya nishati hiyo.

Bwawa la kuzalishia umeme wa maji.
Bwawa la kuzalishia umeme wa maji.Picha: Zhang Zhiwei/Zoonar/picture alliance

Afisa wa Wizara ya Nishati nchini Uganda, Julius Namusaga, ametaja maeneo matatu muhimu yaliyoko kwenye Mto Nile, ambako mitambo hiyo inaweza kujengwa, na mkubwa zaidi ukiwa ni wa Ayago utakaozalisha megawati 840. 

Soma zaidi: Pikipiki za bodaboda Uganda zatoa ajira na vurugu barabarani

Miradi mingine inayolengwa ni mtambo wa Kiba utakaozalisha megawati 400 na Oriang, megawati 392, na kufanya uzalishaji kufikia megawati 3,678 sawa na asilimia 80 ya uzalishaji wa sasa.

Hivi sasa, karibu asilimia 85 ya umeme wa Uganda unazalishwa na vituo vya umeme wa maji, na uliosalia unazalishwa na mitambo ya joto na jua.  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW