1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUganda

Uganda yatafuta ufadhili wa China kwenye ujenzi wa bomba

28 Septemba 2023

Serikali ya Uganda ipo katika hatua za mwisho za majadiliano na wafadhili kutoka China kuisaidia kufadhili mradi wenye utata wa bomba la mafuta ghafi.

Uganda yatafuta ufadhili wa China kwenye ujenzi wa bomba lale la mafuta
Uganda yatafuta ufadhili wa China kwenye ujenzi wa bomba lale la mafutaPicha: ZUMA Wire/IMAGO

Hayo yamesemwa jana na Irene Bateebe katibu katika wizara ya Nishati nchini Uganda.

Akizungumza na shirika la habari la AFP, Bateebe ameeleza kuwa wanafanya majadiliano ya mwisho na washirika wao wa China kuwapa nusu ya fedha za ufadhili wa mradi huo, na kwamba mazungumzo hayo yatakamilika mwezi Oktoba.

Kampuni kubwa ya mafuta ya Ufaransa TotalEnergies inaongoza ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kugharimu mabilioni yad ola kuwezesha Uganda kusafirisha mafuta yake ghafi hadi bandari ya Tanzania, umbali wa kilomita 1, 445.

Mradi huo umekosolewa pakubwa na watetezi wa haki za binadamu na wanaharakati wa mazingira wanaosema utadhuru mifumo ya ikolojia na pia maisha ya maelfu ya watu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW