Uganda yathibitisha kisa kipya cha Ebola
23 Juni 2026
Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, watu 14 wamepona, wagonjwa wanne bado wanapatiwa matibabu hospitalini, huku watu wawili wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo.
Aidha, visa vitano vimeripotiwa nchini Uganda, wakati visa 15 ni vya maambukizi kutoka nje ya nchi . Mamlaka za afya zinaendelea kuimarisha ufuatiliaji na hatua za kudhibiti maambukizi.
Nchini Kongo, ambayo ndio kitovu cha ugonjwa huo wa Ebola, mamlaka zimesema kuwa watu 267 wamefariki toka kuanza kwa ugonjwa huo, miongoni mwa visa 1,048 vilivyothibitishwa hadi kufikia jana Jumatano.
Mlipuko huu wa Ebola unatokana na aina adimu ya virusi vya Bundibugyo ambayo haina chanjo au matibabu rasmi.