1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yatia saini makubaliano ya uwekezaji wa mafuta

Saleh Mwanamilongo
1 Februari 2022

Uganda na kundi la wawekezaji wametangaza uamuzi wao wa kuendelea na uzalishaji wa mafuta kufuatia miaka mingi ya vikwazo vilivyotishia juhudi za nchi hiyo kuwa muuzaji mafuta nje.

Uganda Ölförderung Umwelt Indigene Total
Picha: Jack Losh

Shirika la Kitaifa la Mafuta la China na Kampuni ya Nishati ya Ufaransa TotalEnergies imesema kuwa uwekezaji nchini Uganda utakuwa zaidi ya dola bilioni 10. Kiasi hicho kinajumuisha takriban dola bilioni 3.5 zitakazotumika kujenga bomba la joto linalounganisha maeneo ya mafuta magharibi mwa Uganda na Bandari ya Tanga kwenye bahari ya India nchini Tanzania. Umbali wa maili 897, bomba hilo litakuwa moja ya ndefu zaidi duniani. Uganda inakadiriwa kuwa na akiba ya mafuta inayoweza ya angalau mapipa bilioni 1.4.

Kusainiwa kwa mkataba huo wa uwekezaji ni hatua muhimu ambayo mamlaka ilikuwa na hamu ya kufikia katika miaka 16 tangu wakati huo kiasi cha mafuta kinachoweza kutumika kibiashara kiligunduliwa. Hii inamaanisha wawekezaji wamejitolea kwa dhati kuchimba rasilimali za mafuta ya Uganda na itaendelea kutoa kandarasi kuu.

Soma pia : Rwanda yafungua tena mpaka na Uganda, miaka mitatu baadae

''Nchi sasa inajiamini kuliko kabla''

Juhudi za Uganda kuzalisha mafuta zimetishiwa na madai ufisadi, migogoro ya kodi, na ucheleweshaji wa kiutawala. Hafla hiyo iliofanyika mjini Kampala, mji mkuu wa Uganda iliadhimishwa na shamrashamra, pamoja na maonyesho ya waimbaji wa kikabila na bendi ya polisi. Waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Makamu wa rais wa Tanzania Rais Philip Mpango.

 ''Hii ndiyo siku ambayo Bwana ameifanya,'' ilisema waziri wa Nishjati wa Uganda Ruth Nankabirwa.''Nchi sasa inajiamini kuliko kabla.''

''Tumejitolea kuacha alama chanya ya kimazingira''

Kampuni ya Ufaransa ya TofalEnergies imeahidi kuzingatia ulinzi wa mazingiraPicha: GONZALO FUENTES/REUTERS

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ufaransa ya TotalEnergies, Patrick Pouyanne alisema sherehe hizo ziliashiria muda wa ''kihistoria'' na kuhimiza umoja na uaminifu miongoni mwa washirika wa mradi huo.

Pouyanne alisema ''Pia tunafahamu sana unyeti wa maeneo hayo

ambapo tunakwenda kufanya kazi, hasa kutokana na mtazamo wa kimazingira. Tumejitolea kuacha alama chanya ya kimazingira.''

Mategemeo ya kiuchumi

Soma pia : Shule zafunguliwa Uganda baada ya miaka miwili

Bado haijafahamika ni lini Uganda itauza nje tone lake la kwanza la mafuta, kuanzia kuendeleza maeneo ya kuhifadhi, vifaa vya usafirishaji na miundombinu mingine muhimu itachukua muda.

Mamlaka zinatarajia mauzo ya mafuta kuanza ifikapo mwaka  2025. Licha ya wasiwasi juu ya kushuka kwa bei ghafi katika miaka ya hivi karibuni, matumaini

yamesalia juu nchini Uganda juu ya uwezekano wa mauzo ya mafuta kuinua katika hali ya juu ya kipato cha kati  nchi hiyo ya wakaazi  milioni 45 ifikapo 2040.