1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yatibua shambulizi la bomu kanisani

4 Septemba 2023

Polisi nchini Uganda walifanikiwa kuzima shambulizi la bomu lililokuwa lifanywe na mshambuliaji aliyekuwa amebeba kilipuzi akitaka kuingia kanisani katika mji mkuu, Kampala.

Uganda Kampala Bombenanschlag auf Kirche verhindert
Picha: ABUBAKER LUBOWA/REUTERS

Polisi nchini Uganda wamesema wamefanikiwa kutibua shambulizi la bomu katika kanisa mjini Kampala na kumkamata mwanamume mmoja anayetuhumiwa kwa kujaribu kulipua kilipuzi katika umati wa waumini.

Msemaji wa polisi Patrick Onyango amesema mamia ya waumini waliondolewa kutoka kanisa la Rubaga Miracle Centre katika mji mkuu Kampala baada ya mwanamume kujaribu kuingia katika viwanja vya kanisa hilo akiwa amebeba kilipuzi.

Onyango pia amesema wanawafuatilia wanaume wengine watatu baada ya mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 28, Ibrahim Kintu kufichua huenda alikuwa na watu alioshirikiana nao.

Kanisa hilo lilifungwa watu wasiingie na maafisa wa kikosi maalumu cha kutengua mabomu na mbwa wa kunusa wakafanya upekuzi katika viwanja vyake lakini hakuna kitisho zaidi kilichobainika. Mchungaji wa kanisa hilo Robert Kayanja ameliambia shirika la habari la Ufarana AFP kwamba "bwana amewaokoa kutokana na vifo".

(AFP)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW