Uganda kuzungumza na Tanzania ili kupitisha mafuta yake
15 Februari 2024Uganda haijaridhishwa na mfumo wa muda mrefu ambao kampuni za mafuta za Uganda hununua asilimia 90 ya bidhaa zao kupitia kampuni tanzu za nchini Kenya.
Rais Yoweri Museveni amekuwa akilalamika kuwa hiyo inaiweka nchi yake katika usumbufu wa soko la mafuta na bei za juu za mafuta. Katika kujibu, Uganda ilitangaza kuwa itakabidhi haki za kipekee za usambazaji wa bidhaa zote za mafuta kwa kitengo cha kampuni ya kimataifa ya nishati Vitol.
soma pia:Bomba la mafuta la Afrika Mashariki lakabiliwa na mtikisiko
Uganda ilipanga bidhaa zote ziwasili kupitia Kenya, lakini Waziri Nankabirwa amesema serikali ya Kenya ilikataa kutoa leseni inayohitajika.
Na sasa kamati za kiufundi za Uganda na Tanzania zinafanya mazungumzo. Amesema hivi karibuni atakutana na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kujadili suala hilo.