Ugiriki katika hatari ya kutopata mkopo zaidi
9 Septemba 2016Mkutano huo wa siku mbili unafanyika wakati ambapo Umoja huo wa Ulaya unakabiliwa na ukuaji mdogo wa kiuchumi. Ugiriki ilipokea dola billion 8.5 mwezi juni mwaka huu,ikiwa ni awamu ya tatu ya mkopo wa euro billion 86, kulizuia taifa hilo linalokabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na madeni kurejea tena katika hali ya awali.Kiasi kingine cha euro billion 2.8 kinatazamiwa kutolewa kwa ugiriki , lakini taifa hilo kwanza litahitajika kufanya mageuzi zaidi katika sekta ya ubinafsisaji,benki na hata nishati.
Ugiriki ilikuwa imekubali kuyakamilisha masharti 15 ya wakopeshaji wake kufikia katikati mwa mwezi uliopita lakini haikufanikiwa. Serikali ya Ugiriki yenyewe imeweka bayana inakabiliwa na hali ngumu zaidi, kwani hata pato lake la taifa limeendelea kushuka.Matumaini yake sasa yapo kwa kiasi kikubwa katika Shirika la Fedha Duniani IMF na Umoja wa Ulaya EU, ili kupata usadizi wa kujikwamua katika kipindi kigumu cha kiuchumi na madeni.
Uhispania na Ureno zashindwa kupunguza pengo katika bajeti.
Kwingineko benki kuu ya ulaya imezitaka nchi za Umoja wa Ulaya zinazotumia sarafu ya Euro kujitahidi kuimarisha misingi yake ya kiuchumi. Nayo mataifa ya Uhispania na ureno bado yanakabiliwa na kibarua cha kupunguza pengo katika bajeti zao japo zilifanikiwa kuepuka kutozwa faini mwezi julai mwaka huu kwa kuvunja sheria ya kiwango cha nakisi ya bajeti kilichokubaliwa na umoja wa ulaya.
Chini ya mapendekezo ya tume ya ulaya,umoja wa ulaya uliafikia kutozi adhibu serikali za mjini Madrid na Lisbon kwa kupunguza nakisi zake za bajeti,chini ya kiwango cha umoja huo cha asilimia 3 ya pato la taifa.
Hata hivyo uamuzi huo unaotolewa baada ya msamaha mwingine dhidi ya Ufaransa mwaka uliopita, baada ya kuvunja sheria hiyo ya kiwango cha nakisi ya bajeti kilichowekwa na umoja wa ulaya inazua mashaka mapya ,iwapo zitafanikiwa sheria za bajeti ya umoja huo ,zilizoongezwa makali wakati wa mgogoro wa majuzi wa uchumi.
Mwandishi:Jane Nyingi/AP/RTRE
Mhariri:Saumu