Ugiriki: Wahamiaji 550,000 wako Libya wakisubiri kuja Ulaya
10 Mei 2026
Hayo yameelezwa Jumapili na Waziri wa Uhamiaji wa Ugiriki Thanos Plevris aliyeongeza kuwa serikali mjini Athens kwa ushirikiano na shirika la udhibiti wa mipaka la Umoja wa Ulaya Frontex, pamoja na mamlaka za Libya wameanzisha mkakati wa kupambana na safari hizo na kukabiliana na magenge yanayowasafirisha watu hao kimagendo.
Siku ya Jumapili, walinzi wa pwani wa Ugiriki wamewaokoa wahamiaji 125 waliokuwa katika boti ndogo mbili zilizopatikana pwani ya kusini ya Krete, huku kukitarajiwa kuwasili kwa boti zingine za wahamiaji kutoka Libya.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, mwaka jana, wahamiaji wapatao 42,000 waliwasili katika visiwa vya Ugiriki huku watu 107 wakiripotiwa kufa maji katika bahari ya Mediterania.