1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki yaendelea kupambana na moto mkali wa nyika

13 Agosti 2024

Ugiriki leo inapambana na moto mkubwa wa nyika karibu na mji mkuu, Athens, kwa siku ya tatu mfululizo huku mamia ya wazimamoto wa Ulaya wakitarajiwa kujiunga na juhudi hizo za kuudhibiti moto huo.

Ugiriki| Moto wa nyika
Ndege ikijaribu kuzima moto kwa maji UgirikiPicha: Alexandros Avramidis/REUTERS

Ugiriki leo inapambana na moto mkubwa wa nyika karibu na mji mkuu, Athens, kwa siku ya tatu mfululizo huku mamia ya wazimamoto wa Ulaya wakitarajiwa kujiunga na juhudi hizo za kuudhibiti moto huo, ulioteketeza sehemu ya maeneo ya mji mkuu huo. Mtu mmoja amefariki dunia na angalau wengine 66 kutibiwa kutokana na majeraha.

Maafisa wawili wa zimamoto pia wamejeruhiwa. Maafisa 700 wa zimamoto wakisaidiwa na wahandisi 200 na ndege tisa, wote wanapambana na moto huo leo, ulioanza siku ya Jumapili. Ukiwa umezidishwa na upepo mkali, moto huo mbaya zaidi kuikumba Ugiriki mwaka huu umesababisha maelfu ya watu kuyakimbia makaazi yao. Shirika la utabiri wa hali ya hewa huko Ugiriki limesema mji wa Athens leo unatarajia joto kufikia nyuzi 38 katika vipimo vya Celsius na upepo utakaovuma kwa kasi ya kilomita 39 kwa saa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW