1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki yataka msaada wa Umoja wa Ulaya na IMF

27 Aprili 2010

Ugiriki inahitaji msaada wa dharura wa fedha, ama sivyo serikali itashindwa kulipa madeni yake

Greek Finance Minister George Papaconstantinou speaks during a media conference after a meeting of EU finance ministers in Madrid, on Saturday, April 17, 2010. European Union finance ministers were working Saturday on ways to ensure tougher banking supervision, and considering a bank levy to pay for banks that collapse in the future, hoping to prevent a repeat of the recent financial crisis which cost governments billions of euros. (AP Photo/Virginia Mayo)
Waziri wa Fedha wa Ugiriki, George PapaconstantinouPicha: AP

Waziri wa Fedha wa Ugiriki, Giorgos Papakonstantinou alitamka hayo katika hotuba yake bungeni mjini Athens. Amesema,deni la Euro bilioni 9 linapaswa kulipwa na serikali ifikapo tarehe 19 mwezi Mei.

Wakati huo huo vyombo vya habari nchini Ugiriki vimeripoti kuwa waziri Papakonstantinou alizungumza kwa simu pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, lakini havikueleza yale yaliyojadiliwa.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: DW

Hata hivyo mjini Berlin, Kansela Merkel na waziri wa fedha Wolfgang Schäuble wamesisitiza kuwa uamuzi wa msaada huo utapitishwa baada ya kukamilishwa majadiliano yanayofanywa kati ya Kamisheni ya Ulaya, Shirika la Fedha la Kimataifa- IMF na serikali ya Ugiriki.

Mpango unaojadiliwa unahusika na mikopo ya dharura ya hadi Euro bilioni 45.Umoja wa Ulaya unatazamiwa kutoa Euro bilioni 30 huku Ujerumani pekee ikichangiaa Euro bilioni 8.4. Na Euro bilioni 15 zingine zitatoka kwa IMF.

Mwandishi:Martin,Prema/DPA

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW