1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki yawapa hifadhi watoto wasioambatana na wazee wao

27 Julai 2023

Shirika la misaada la Save the Children limesema chini ya theluthi moja ya watoto ambao hawajaandamana na wazazi wao walifanikiwa kupata hifadhi nchini Ugiriki mwaka uliopita, huku maombi mengine mengi yakikataliwa.

Griechenland Eleonas Flüchtlingslager
Picha: Aristidis Vafeiadakis/Zuma/picture-alliance

Shirika hilo limetoa wito wa kuwalinda wale walio hatarini zaidi.

Ugiriki ni moja ya njia kuu za kuingia katika Umoja wa Ulaya kwa wakimbizi na wahamiaji kutoka Mashariki ya Kati, Afrika na Asia.

Soma zaidi: Boti yazama Mediterrania, 400 wahofiwa kuangamia

Katika taarifa yake iliyoitoa leo, Save the Children imesema kwamba maombi ya hifadhi 981 kati ya 3,175 yaliwasilishwa Ugiriki mwaka jana na watoto ambao hawajaandamana na wazazi wao, wenye hadi umri wa miaka 18, yalikubaliwa.

Shirika hilo limesema watoto wasio na nyaraka wanaishi katika hali ya kutojiamini na hofu ya kufukuzwa
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW