Ugomvi wa wazazi na athari za kisaikolojia kwa watoto
8 Agosti 2013Matangazo
Ulevi, usaliti, hali ngumu ya maisha na tabia ya kiburi vinatajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vya migogoro ya majumbani na ambayo husababisha watoto kupoteza mapenzi kwa wazazi wao na hata kujenga tabia ya kisasi, ambayo nayo inaweza kuja kuwaathiri watoto wao watakapokuwa watu wazima.
Ambatana na Hashim Gulana kwenye makala hii ya Mbiu ya Mnyonge kujifunza mengi juu ya kadhia hii inayoweza kuepukwa na hivyo kuwasaidia watoto kupitisha utoto wao kwa salama.
Makala: Hashim Gulana
Mhariri: Mohammed Khelef