Janga
Ugonjwa usiofahamika wauwa watu 143 DRC
3 Desemba 2024Matangazo
Watu walioambukizwa walikuwa na dalili za kuugua mafua pamoja na kupata joto kali mwilini na kuumwa kichwa. Kwa mujibu wa maafisa hao wa ngazi za juu Kongo, timu ya madaktari imepelekwa katika kitengo maalum cha afya cha Panzi kuchukuwa sampuli na kuanzisha uchunguzi, kutambuwa ugonjwa huo.
Kiongozi mmoja wa shirika la kiraia Cephorien Manzanza ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba hali inatiwa wasiwasi mkubwa kufuatia kiwingu cha kuongezeka kwa idadi ya walioambukizwa.
Mtaalamu mmoja wa magonjwa ya mripuko kwenye eneo hilo amesema wengi walioambukizwa ni kina mama na watoto.