Ugumu wa safari ya wakimbizi kuja Ulaya
1 Septemba 2015Matangazo
Macedonia si miongoni mwa nchi maarufu duniani. Lakini katika siku za hivi karibuni imekuwa ikigonga vichwa vya habari mara kwa mara kwa sababu ni moja ya nchi ambazo wakimbizi wanazipitia wakitaka kuingia katika Umoja wa Ulaya. Inakadiriwa kwamba zaidi ya wahamiaji laki moja wamefunga safari kutokea Ugiriki na kwenda Macedonia, Serbia na baadae Hungary katika juhudi za kupata hifadhi.
Mwandishi wa DW Nemanja Rujevic ameambatana na wakimbizi hao na kusikia visa vyao katika safari ndefu ya kukimbia vita na adha huko wanakotokea. Simulizi yake mnaletewa na Elizabeth Shoo katika Mwangaza wa Ulaya.
Kusikiliza kipindi bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.