1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhaba wa maji Turkana, Kenya

22 Machi 2022

Jimbo la Turkana nchini Kenya, limeongeza juhudi za kupambana na uhaba wa maji ambao umedumaza huduma muhimu kwa binaadamu jimboni humo. Serikali ya Jimbo hilo sasa inatumia maji ya ardhini kuwasaiida wakaazi

BG Kenia Turkana Kriger
Picha: Reuters/G. Tomasevic

Serikali ya Jimbo hilo sasa inatumia maji ya ardhini kama sehemu ya juhudi zake za kuwakwamua wakaazi wa eneo hilo ambao ni wafugaji na pia imekuwa ikichimba visima na mabwawa ya maji kuuangamiza uhaba huo.

Huku ulimwengu ukiwa umeadhimisha siku ya maji mnamo jumatatu, ukosefu wa maji katika kaunti ya Turkana umeendelea kuwakosesha amani wakaazi ambao wamekuwa wakilazimika kusafiri kilomita kadhaa kutafuta bidhaa hiyo adimu.

Serikali ya Jimbo la Turkana, imekuwa ikipokea mgao mkubwa wa fedha kutoka kwa serikali ya kitaifa kuangazia changamoto ya ukosefu huo miongoni mwa zingine japo hali imeonekana kusalia vivyo hivyo.

Kwa mujibu wa afisa mkuu wa idara ya maji wa Turkana Moses Natome,suluhu la ukosefu wa maji Turkana litapatikani hivi karibuni.

Kulingana naye,uzinduzi wa chemichemi ya maji eneo la Napuu ni mpango mwafaka wa kupata suluhu la maji.Aidha,ameeleza kwamba,iwapo watapata fedha Zaidi,wanakusudia kuchimba maji na kuwasambazia wakaazi katika maeneo athirika. "Tumegunduwa kwamba,kila mwananchi anaweza kuwa na maji. Kile kinahitajika ni kuwekeza fedha ili kuwasambazia wakaazi maji." Anasema Natome.

Waziri wa afya serikali ya jimbo la Turkana Jane AjelePicha: UNCCD Kenya

Baadhi ya wakaazi wa Turkana wameelezea matumaini yao kufuatia uzinduzi wa chemichemi hiyo ya maji ambayo inakusudia kuwafikia zaidi ya watu elfu kumi na mbili.

Huyu hapa ni mkaazi wa kalokol viungani mwa mji wa lodwar. "Kupata maji wakati huu ni ngumu kabisa.Hali imekuwa kwa muda mrefu na tumeteseka na hii serikali imeshindwa kutusaidia sisi waturkana" Anasema mkaazi mmoja.

Waziri wa afya katika serikali ya jimbo la Turkana Jane Ajele, amekiri kwamba,ukame umeaathiri watu wengi huku akibaini kwamba,watoto ndio waathiriwa wakuu wa ukame na ukosefu wa maji.

Waziri Ajele kadhalika ametaja visa vya utapiamlo vinavyoshuhudiwa wakati huu hapa Turkana kama iliyochochewa na ukosefu wa lishe na maji. "Tunavyoona hapa,kati ya Watoto watano mmoja wao ameathirika na ukame nah ii ni kama asili mia ishirini nukta nne..” Ajele

Serikali ya Jimbo la Turkana hutenga kati ya shilingi milioni nne na Tano Kila mwaka wa kifedha kushugulikia tatizo la uhaba wa maji.

Kwa sasa,wakaazi wanaendelea kuwa na matumaini ya kupata maji licha ya ukame unaoeshuhudiwa wakati huu.

Michael Kwena, DW Lodwar

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW