Uhalisia wasambaratisha uongo wa Trump kuhusu corona
2 Oktoba 2020Kwa miezi kadhaa Trump amepuuza hatari za ugonjwa wa Covid-19, kuwakejeli watu wanaojaribu kujilinda kwa kuvaa barakoa, kuutaja ugonjwa huo hatari kama ulioletwa na chama cha Democratic, na kudai kwamba hali si mbaya kihivyo.
Ingawa siyo rahisi kueleza mapema baada ya kutangazwa kwa matokeo ya vipimo, iwapo na kwa namna gani rais huyo mwenye umri wa miaka 74 ataugua, athari za kampeni ya kisiasa ziko wazi sana wakati uchaguzi ukikaribia: Itakuwa janga.
Bila kujali hasara
Majaribio yote ya kuondoa nadhari kwenye kushindwa kwake, ukweli kwamba hakuna mkakati wa kitaifa wa kuwalinda raia, kwamba magavana wameachwa peke yao na wakati huohuo zaidi ya Wamarekani laki mbili wamefariki kutokana na ugonjwa huo, yote hayo yamekuwa batili.
Soma pia: Viongozi wa dunia wamtakia afueni Trump
Uhalisia umesambaratisha uongo wote wa rais. Yeye pamoja na maafisa wake hawatafanikiwa tena kuwasha mishumaa ya moshi, katika kuyawasilisha maandamano ya vurugu kwenye baadhi ya miji kuwa hatari zaidi ya ukweli kwamba Wamarekani 1000 hufa kila siku kutokana na virusi hivyo.
Kwa nguvu zake zote na bila kujali hasara, Donald Trump amejaribu kuufufua uchumi kabla ya siku ya uchaguzi. Kwa tukio hili la kuambukizwa virusi, mpango huu pia umekuwa batili. Hata wakanushaji wa corona hawataweza sasa kuepuka kukiri kwamba virusi hivyo vina uwezo mkubwa wa kusambaa - ikiwa vimeweza kumfikia hata mtu mwenye nguvu aliyoko ikulu ya White House. Oktoba 2, nchi hiyo iko mbali kuliko wawati wowote ule, na utulivu ambao Trump amekuwa akihaha kuuwekea matumaini.
Soma pia:Maoni: Trump aongeza joto kwa kupendekeza kusogeza uchaguzi
Nadharia za uovu na njama
Mara baada ya habari za maambukizi yake kuwekwa hadharani, wimbi la taarifa za kumtakia shari rais huyo limeenea, hadi kufikia dhana kwamba maambukizi hayo ni njama aliyoibuni ili kuondoa nadhari kwenye uchunguzi wa maoni ya wapigakura unaoonesha kushuka vibaya kwa umaarufu wake.
Soma pia: Trump na mkewe waambukizwa virusi vya corona
Anaweza kushughulikia haya. Rais huyo amezowea kuwa na ukweli mbadala. Lakini siyo na kupoteza sifa yake ya askari shupavu. Kwa sababu hiyo inamaanisha hakuna mengi aliyobakisha.
Biden ghafla siyo mzee tena, bali muangalifu
Baada ya mdahalo wa kwanza wa televisheni, hoja kuu ya wafuasi wa Trump ilikuwa kwamba yeye ni imara zaidi na hivyo ndiye anafaa kwa ofisi ya rais inayochosha kuliko mpizani wake. Ikiwa Joe Biden pia hakuambukizwa wakati wa mdahalo huo, hoja hii - alau kwa wiki zijazo, haitakuwa tena na mashiko. Sasa siyo tena udhaifu wake utakaotumiwa, bali busara zake kuhusu umri wake, ambao unaelezwa kwa tahadhari.
Soma pia: Harris atokea kwa mara ya kwanza kwenye kampeni
Trump dhaifu hana kingine zaidi cha kutoa. Na bila shaka siyo kiongozi sahihi wa kupambana dhidi ya janga hatari la maambuzi. Uungwana unatulazimu tumtakie Trump na mke wake Melania kila la kheri katika siku zijazo.