1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiga kura wa Ujerumani waamua kuchagua mabadiliko

27 Septemba 2021

Wajerumani wakataa kuongozwa na muungano uliopita wa vyama vikubwa kwa kuviinua vyama vidogo kutetea agenda wanazozipendelea

Wapiga kura wa Ujerumani wameutikisa mwelekeo wa kisiasa katika nchi hii. Wameamua kuukataa kabisa muungano wa vyama vikuu vya CDU/CSU na SPD kuhodhi madaraka. Mhariri mkuu wa Dw Manuela Kasper-Claridge anasema Wajerumani wameamua kuchagua  mabadiliko.

Mabadiliko yameshawasili, maamuzi ya wapiga kura wa Kijerumani yako wazi kabisa, ahadi za ubabaifu za muungano uliopita wa vyama vikuu zimefikia kikomo chake. Na sasa ni wakati wa kuzitazama changamoto muhimu za kulinda mazingira, kuifanya Ujerumani kuwa nchi ya kidijitali na haja ya kuifanya nchi hii kuwa ya kisasa.

Majukumu haya yanaweza tu hivi sasa kutafutiwa ufumbuzi na kufanikishwa na serikali itakayovishirikisha vyama vidogo. Kwa yeyote atakayeunda serikali mpya ya Ujerumani hapana shaka atalazimika kushirikiana na chama cha Kijani sambamba na Waliberali wa chama cha Free Democratic FDP.

Mhariri mkuu wa DW-Manuela Kasper-ClaridgePicha: DW/M. Altmann

Vyama vyote hivyo ni sauti muhimu katika serikali ijayo. Kwa maneno mepesi ni kusema bila ya vyama hivyo hakuna kitakachowezekana. Na bora hivyo. Na  yawezekana hatimae ukapatikana mwelekeo mpya wa waliberali wenye msimamo wa wastani. Kupigiwa kura kwa wingi cha cha walinda mazingira imeonesha wazi kwamba Wajerumani walio wengi wana khofu na mabadiliko ya kimazingira.

Na kwa matokeo ya uchaguzi huu hata chama cha Kijani kitaingia kwenye mazungumzo ya kutafuta serikali ya mseto kwa kujiamini kabisa. Ushindi huu umekipa chama hicho turufu kubwa na kinaweza kushinikiza madai yake. Hata hivyo inawezekana Wajerumani wakawa ni watu wasiokuwa tayari kwa mabadiliko kama kilivyotarajia chama cha kijani na kiongozi wake bibi Annalena Baerbock, na hasa kutokana na kuonesha pia kwamba mabadiliko yanayotakiwa yanahitaji fedha.

Kwa upande mwingine chama cha FDP ni muhimu kwenye serikali ijayo kwa sababu haitowezekana kuunda serikali bila ya chama hicho. Chama hiki cha Waliberali kinachitazama kama wasawazishaji muhimu wa mambo,na wanaweza kuyazima baadhi ya matakwa ya wanamazingira.

Chama cha FDP kinaweka imani kubwa kwenye soko,dijitali na kupunguza ukiritimba. Wanakubaliana na suala la kuyalinda mazingira lakini sio kwa gharama ya kuongezwa kodi. Na kwa namna gani hilo linavyoweza kufanyika, ni suala ambalo watalazimika kulifafanua pale watakapoingia kwenye mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto. Ama kwa wana CDU/CSU kilichoonekana ni bayana kwenye matokeo ya jana ni kuporomoka hasa kusikokuwa na mithili.

Japokuwa chama hiki kilipoteza kura chache tafauti na makadirio ya awali lakini huwezi kukipamba kwa matokeo mabovu yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huu wa shirikisho.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW