1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumano inadorora katika suala la mabadiliko ya tabanchi

Oumilkheir Hamidou
15 Mei 2019

 Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi umeitishwa Berlin. Ujerumani iliyokuwa ikisifiwa kuwa na "kansela wa mazingira", imebadilika na kukosolewa kuwa mchafuaji mkubwa wa mazingira.

Kommentatorenfoto Jens Thurau
Picha: DW

Miaka takriban kumi baada ya mkutano wa Umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi mjini Kopenhagen, serikali ya Angela Merkel imekaa kimya vya kutosha katika suala la mabadiliko ya tabianchi. Mkutano huo ulioitishwa katika mji mkuu wa Danemark ambapo mkataba mpya kuhusu mabadiliko ya tabianchi ulitarajiwa kutiwa saini, ulishindwa vibaya sana. China na Marekani walijadiliana kuhusu mada hiyo lakini sio kuhusu namna ya kupunguza moshi unaotoka viwandani. Nchi zinazoinukia zinalalama. Kansela aliyekasirika aliondoka mkutanoni usiku wa manani , hakuweza kuficha hasira zake kuelekea uzito wa nchi za viwanda.

Baadae serikali kuu ya Ujerumani ikatafakari pamoja na mataifa mengine na kubuni aina ya "Kundi la watiifu",nchi ambazo hazikujiachia kushawishiwa na hali ya uzito ya Marekani na China kuelekea mabadiliko ya tabianchi.Tangu wakati huo wamekuwa wakiitisha "kongamano la Petersburg"-ambalo safari hii limeitishwa kwa mara ya kumi mjini Berlin.

Na mnamo mwaka huu wa 2019 kongamano hilo limebainisha jinsi mambo yanavyobadilika kila wakati unapopita.

Majiani vijana wanaohudhuria kongamano hilo wamejionea kinachotokana na kutofanywa chochote kukabiliana na madhara ya moshi unaotoka viwandani. Katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita hakuna makubwa yaliyotekelezwa Ujerumani kuelekea mada hiyo. Si haba kwamba rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amependekeza hivi karibuni, mataifa ya Ulaya yaahidi kulifikia lengo la kusawazisha mabadiliko ya tabianchi hadi ifikapo mwaka 2050-ikimaanisha wapunguze moshi wa viwandani kulingana na kiwango  cha hewa safi inayopatikana misituni.

Mataifa manane yamejiunga na mkakati wa Ufaransa. Ila Ujerumani. Na Merkel anashikilia msimamo ule ule wa hotuba yake katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi:Yaani kwanza njia kuelekea "hali sawia ya mabadiliko ya tabianchi" itakapojulikana ndipo nayo Ujerumani itakapojiunga na mkakati huo. Na sio kabla.

Merkel anakumbusha juhudi zote zilizoanzishwa na Ujerumani ulimwenguni; kitita cha Euro bilioni moja na nusu kwaajili ya fuko la mabadiliko ya tabianchi, na misaada kwa nchi masikini. Kansela anataka hakikisho juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi zinaendelea. Lakini dalili zinazoonyesha  kwamba Ujerumani, ambayo wakati mmoja ilikuwa mshika bendera wa juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, wamezitafuta wawakilishi wa mataifa 35 waliohudhuria kongamano hilo la mjini Berlin,lakini hawakuzipata.

 

Mwandishi: Thurau Jens/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Josephat Charo