Uhispania mabingwa wapya dunia
12 Julai 2010Matangazo
Bao hilo lilifungwa na Andreas Iniesta dakika chache kabla ya kumalizika kwa muda wa nyongeza, baada ya timu hizo kutoka suluhu katika muda wa kawaida. Uhispania pia ndiyo mabingwa wa Ulaya
Wakati huo huo mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller amekuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kutokana na mabao matano aliyofunga.Pia Muller ameteuliwa kuwa mchezaji bora kijana katika michuano hiyo.Diego Follan wa Uruguay alichaguliwa kuwa mwanasoka bora.
Kabla ya kuanza kwa pambano hilo la fainali kati ya Uholanzi na Uhispania, Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliingia katika uwanja wa Soccer City akiwa kwenye gari la wazi ambapo alishangiliwa sana wakati alipozungushwa kuwasalimia watazamaji.
Mwandishi:Aboubakary Liongo