Uhispania: Maelfu waandamana kudai nuymba za bei nafuu
14 Oktoba 2024Chini ya kauli mbiu "Nyumba ni haki, sio biashara" waandamanaji walitoa wito wa kupunguzwa kwa kodi na kuimarishwa kwa hali ya maisha.
Serikali inakadiria kuwa takriban watu 22,000 walishiriki katika maandamano hayo ijapokuwa waandaji wanadai kuwa watu wanaofikia 150,000 walishiriki.
Soma pia:Maelfu waandamana kupinga mipango ya kaimu waziri mkuu Sanchez nchini Uhispania
Mnamo mwezi Julai, serikali ya Uhispania ilitangaza msako dhidi ya nyumba za kuishi kwa muda ama pia za likizo za muda mfupi kuthibitisha kama zina leseni za kukodisha.
Katikamaandamano tofauti huko Barcelona, raia tayari wamelalamika dhidi ya utalii wa kupita kiasi katika mji huo maarufu wa pwani.
Sasa wanahoji uamuzi wa mamlaka kuandaa Kombe la Amerika mwishoni mwa msimu wa kiangazi unaoshuhudia watalii wengi.