Uhispania na Sweden kukutana nusu fainali Kombe la Dunia
11 Agosti 2023Timu za taifa za wanawake za Uhispania na Sweden zimetinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea huko nchini Australia na New Zealand.
Soma zaidi: Sweden yawaondoa mabingwa watetezi Kombe la Dunia la Wanawake
Uhispania imeweka rekodi mapema leo ya kuwa la kwanza kufika nusu fainali la Kombe la Dunia kwa wanawake kwa mwaka 2023 kwa kuwatoa washindi wa pili wa kombe hili wa mwaka 2019 Uholanzi wkwa kuwafunga 2-1 katika mchezo mgumu ulioendab hadi dakika 120.
Nyota wa Uhispania Salma Paralluelo ameweka rekodi ya kufunga goli liliwapa nafasi Uhispania katika dakika ya 111 ya kufika hatua hiyo huku yeye mwenyewe akiweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga goli katika mashindano ya Kombe la Dunia akiwa na miaka 19 pekee.
Kwa upande mwingine Sweden walikuwa na kibarua cha kumenyana na mabingwa wa mwaka 2011 Japan ambapo Sweden wametinga nusu fainali kwa kuifunga Japan 2-1.
Hadi kipindi cha kwanza kinakamilika Sweden walikuwa wanaongoza kwa goli moja lililotiwa kimiani na Ilestedt katika dakika ya 32, Dakika ya 51 Sweden walipata mkwaju wa penati iliyofungwa na Angeldahl, Dakika ya 87 Japan walipata goli la kufutia machozi lilofungwa na hayashi.
Uhispania na Sweden watakutana siku ya tarehe 15 mwezi huu katika uwanja wa Eden Park katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia la Wanawake 2023.