Michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake imeanza vyema kwa wahispania baada ya kuwalaza wapinzani wao Costa Rica mabao 3-0
Matangazo
Wahispania wameonyesha ni kwa namna gani wao ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa katika mechi yao ya kwanza ya kundi C mjini Wellington, kwa kuwafunga 3-0 ndani ya dakika sita tu, wapinzani wao Costa Rica ambao walitumia takribani mchezo mzima kujilinda.
Bao la kwanza lilipatikana pale mlinzi wa Costa Rica Valeria del Campo alipoinasa krosi iliyomsababishia wao kujifunga kutoka kwa Esther Gonzalez. Huku goli la pili likiwekwa wavuni na Aitana Bonmati na bao la tatu likitundikwa na Esther Gonzalez.
Mchezaji wa Barcelona, Aitana Bonmati alikuwa mchezaji wa kiwango cha juu wakati wote wa shindano hilo, huku akitengeneza nafasi nyingi bora za Uhispania kuweza kupata magoli. Bonmati ni mmoja wa wachezaji watatu waliorejea kutoka uhamishoni kwa miezi tisa kucheza Kombe la Dunia.
Mshindi wa Ballon d'Or
Kocha Jorge Vilda alidokeza kuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or mara mbili wa Uhispania Alexia Putella atakua miongoni mwa wachezaji wa akiba kutokana na jeraha baya la goti huku Bonmati na Esther wakiendeleza mashambulizi kwenye eneo la hatari la Costa Rica.
Kipa wa Costa Rica Daniela Solera, aliokoa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Jennifer Hermoso, katika kipindi cha kwanza na akiingia kati mara kadhaa, lakini hiyo haikuwa tija kwa Wahispania ambao walipanda kileleni mwa kundi lao kabla ya mchezo wa Japan dhidi ya Zambia siku ya Jumamosi.
Timu hizo ziliwahi pia kutoka sare ya mabao zilipovaana katika mechi yao ya kwanza yaKombe la Dunia mwaka 2015. Uhispania kwa sasa iko nafasi ya sita katika viwango vya ubora wa wanawake na imeonyesha uwezo wake wa kiufundi kwa kuifunga Costa Rica mara tatu katika dakika sita mfululizo.
Tazama:
Wajue wanawake 10 mahiri zaidi wa soka duniani
Wanawake wa Ujerumani watauanza msimu wa 2019 kwa mechi ya kirafiki na Ufaransa ambaye ni mwenyeji wa kombe la dunia. DW inawatambulisha wanawake 10 bora kwenye soka, kwa kuzingatia uteuzi wa tuzo za FIFA za Ballon d'Or.
Picha: Reuters/G. Garanich
Ada Hegerberg - Mshambuliaji wa "dhahabu"
Ni mshambuliaji wa Norway. Historia yake inaanzia mwaka 2018 baada ya kushinda tuzo ya Ballon d'Or ya wanawake. Akiwa na miaka 23 aliwavutia wasichana wadogo wakati wa hafla tuzo hizo: "Tafadhali, jiamini." Hegerberg, anayetambulika kwa mashuti na mipira ya vichwa amefunga mabao zaidi ya 250 na alishinda mara tatu ligi ya mabingwa, na makombe manne ya ligi ya Ufaransa.
Picha: picture-alliance/NTB Scanpix/V. Wivestad
Pernille Harder - Mmaliziaji hatari.
Fainali za Euro za Wanawake 2017: MDenmark, Pernille Harder alipambana juu chini na kufanikiwa kusawazisha mabao hadi 2-2 katika mechi ambayo Denmark ilipoteza kwa mabao 4-2. Ulikuwa ni ujuzi kama huu uliompafanya kuwa mfungaji bora wa timu ya Wolfsburg wanawake na mchezaji bora kwenye ligi ya wanawake ya Bundesliga 2017-18 - na Mchezaji bora wa mwaka wa UEFA Wanawake.
Picha: Reuters/Y. Herman
Wendie Renard: Mlinzi mahiri.
Wendie Renard akiwa na Olympique Lyon na timu ya wanawake ya Ufaransa. Kutokana na ujuzi wake wa kujilinda na magoli yasiyo ya kawaida, kiungo huyo wa nyuma ameshinda mara 11 ligi ya Ufaransa na Ligi ya Mabingwa mara nne mfululizo. Renard anaonekana mmoja wa walinzi bora wa kike duniani, na anaahidi kuwa sehemu muhimu ya kampeni za Les Bleues kushinda Kombe la Dunia la Wanawake 2019 nyumbani.
Picha: Getty Images/AFP/Jonathan Nackstrand
Lucia Roberta: Mchezaji muhimu
Mlinzi mahiri wa klabu yake ya Oympique Lyon Lucy Bronze aliyenga'ra dhidi ya klabu yake ya zamani ya Man. City kwenye nusu fainali za ligi ya klabu bingwa ya wanawake mwaka 2018, aliteuliwa kwenye tuzo za goli bora zaidi la msimu kwenye UEFA.com. Bronze anachukuliwa kama mwanasoka bora zaidi mwanamke duniani na kuahidi kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Uingereza kwenye Kombe la Dunia 2019.
Picha: Getty Images/N. Baker
Marta Vieira da Silva: 'Nilizaliwa kutumia hiki kipaji'
"Pambana dhidi ya ubaguzi. Pambana na ukosefu wa msaada. Pambana dhidi ya kila kitu - wavulana, watu ambao wanasema huwezi," Marta aliandika katika makala kwenye jarida la The Tribune Players. Kwa uwezo huu, ujuzi wake wa "samba" na magoli yake 110 katika mechi 133 kwa Brazil, fowadi wa Orlando Pride, Marta anaonekana kama mchezaji bora zaidi wa kike duniani na shujaa kwa wasichana wengi wadogo.
Picha: Getty Images
Dzsenifer Marozsan - Kurejea baada ya kuugua mapafu
Ilikuwa Julai iliyopita tu nahodha wa zamani wa Ujerumani na kiungo wa Olympique Lyon alipata maradhi ya mapafu. Mwezi Oktoba alirudi tena kwenye klabu yake, na mwezi mmoja baadaye alijiunga na timu yake ya kitaifa. Marozsan ni mchezaji ambaye hutoa huduma nzuri kwa wenzake wa mbele. Akiwa amecheza michezo 347 na magoli 134, Marozsan inaonekana kama mmoja wa wachezaji watatu bora zaidi duniani.
Picha: picture-alliance/GES/T. Eisenhuth
Amandine Henry - Mnyakuaji hatari wa mipira
Karibu kila mpira hupitia kwa kiungo huyu mshambuliaji wa Ufaransa Amandine Henry (juu, kulia). Huapata mpira kwa haraka na kuupeleka mara moja kwa mshambuliaji akiwa na timu yake ya Ufaransa na klabu yake, Lyon. Kutokana na namna anavyousoma mchezo, ndivyo anavyochukuliwa kama mmoja wa washambuliaji wakali zaidi wa kike duniani.
Picha: Reuters/V. Ogirenko
Samantha Kerr – Anatambulika kwa sarakasi za "somersault"
Samantha Kerr ana rekodi ya magoli 55 katika michezo 94 katika ligi ya Taifa ya Wanawake ya soka nchini Marekani. Kerr alianza na timu ya taifa ya wakubwa ya Australia akiwa na umri wa miaka 15. Tangu wakati huo ameiongoza Matildas hadi kuwa ya sita katika viwango vya FIFA vya wanawake na kufuzu kwa kombe la Dunia kwa Wanawake, 2019. Anafurahia kila goli akiwa na sarakasi zake za somersault.
Picha: Getty Images/G. Denholm
Megan Rapinoe - Mtafutaji magoli
Winga Megan Rapinoe aliisaidia Marekani kushinda michuano ya SheBelieves 2018, Kombe la Dunia, 2015 na medali ya dhahabu katika Olimpiki za 2012. Kapteni huyo wa Seattle Reign alifunga mabao 12 kwenye michezo 18 mwaka 2017. Megan ni kivutio kwa wasichana wengi ulimwenguni, anayepigana dhidi ya ubaguzi na hutoa asilimia moja ya mshahara wake kwenye shirika la misaada la Common Charitable.
Picha: Getty Images/R. Martinez
Saki Kumagai - Kito cha WaJapan
Nahodha wa Japan. Ameshinda katika makombe matano ya Ufaransa na matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa akiwa na Olympique Lyonnais. Ujuzi wa kujihami wa Saki ulisaidia Japan kushinda kombe la wanawake Asia mwaka 2018. Alifunga bao la ushindi kwa penati na kunyakua kombe la dunia la 2011 dhidi ya Marekani. Aliteuliwa kwenye kipengele cha mchezaji bora wa kike kwenye tuzo za FIFA.