Uhispania yalenga kufuta mashaka Kombe la Dunia
21 Juni 2026
Mabingwa wa Ulaya Uhispania wanatarajia kurejea kwenye kiwango bora watakapocheza dhidi ya Saudi Arabia leo katika michuano ya Kombe la Dunia la 2026baada ya kutoka sare tasa na Cape Verde kwenye mchezo wao wa kwanza.
Kocha Luis de la Fuente amesema wachezaji wake wameguswa na ukosoaji waliopata na wana dhamira ya kuonyesha uwezo wao halisi. Haya yanajiri huku mashabiki wakitarajia kuona iwapo Lamine Yamal ataanzishwa katika kikosi cha kwanza.
Katika mechi nyengine hii leo Ubelgiji itamkosa tena Jeremy Doku kutokana na matatizo ya kupumua wanapokutana na Iran, huku Iran ikilalamikia vikwazo vya safari vilivyoathiri maandalizi yao.
Kocha wa Iran Amir Ghalenoei amesema ameambiwa kuwa masharti ya safari ya Marekani kwa timu yake yatalegezwa hatimaye kuelekea mchezo wao wa tatu wa makundi dhidi ya Misri mjini Seattle Juni 26, lakini amedai kuwa namna walivyotendewa hadi sasa imeathiri vibaya matokeo yao uwanjani.