Uhispania yanyakua ubingwa wa EURO 2024
15 Julai 2024Matangazo
Kocha wa timu ya taifa ya Uhispania Luis de la Fuente amewashukuru wachezaji wake kwa kuweka rekodi ya kushinda taji lao la nne la mashindano ya soka ya Ulaya ya Euro.
De la Fuente aliirithi nafasi ya Luis Enrique baada ya timu ya Uhispania kuondolewa katika Kombe la dunia la mwaka 2016 kwenye duru ya mtoano ya 16 bora huku wengi wakikosa matumaini kwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 63.
Baada ya kushindwa na Scotland katika mechi za kuwania kufuzu mashindano ya Euro mnamo mwezi Machi mwaka jana, baadhi ya vyombo vya habari vilisema kwamba ataachishwa kazi.
Lakini timu hiyo iilijipanga vyema na haijashindwa tangu wakati huo na sasa ni mabingwa wapya wa soka, Ulaya mwaka 2024.