1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhispania yapitisha sheria ya kubadilisha jinsia

16 Februari 2023

Wabunge nchini Uhispania hii leo wamepitisha sheria ya kubadilisha jinsia inayoruhusu mtu aliyefikisha umri wa miaka 16 na zaidi kubadilisha jinsia yake kwenye kitambulisho, licha ya hatua kama hiyo kuibua mgawanyiko.

Spanien Madrid | Terrasse einer Bar
Picha: Pablo Blazquez Dominguez/Getty Images

Uhispania sasa inakuwa moja ya mataifa machache yanayoruhusu watu kubadilisha jinsia kwenye vitambulisho vya taifa kwa kufuata mchakato mwepesi wa kutangaza mabadiliko. 

Bunge hilo pia limetoa idhini ya mwisho kwa sheria inayoruhusu likizo ya malipo ya matibabu kwa wanawake wanaopata maumivu makali wakati wa hedhi na kuwa taifa la kwanza barani Ulaya kuwa na sheria ya aina hiyo.

Soma pia:Dani Alves atuhumiwa kwa kumnyanyasa kingono mwanamke

Hatua hiyo lakini imeibua mgawanyiko miongoni mwa wanasiasa na vyama vya wafanyakazi, huku chama kikubwa cha wafanyakazi cha UGT kikionya inaweza kusababisha wanawake kunyanyapaliwa na wanaume wengi zaidi kuajiriwa. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW