1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhispania yasusia kuapishwa rais wa Mexico

25 Septemba 2024

Uhispania imetangaza kususia sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Mexico, Claudia Sheinbaum, kwa kuwa Mfalme Filipe wa Sita hakualikwa.

Rais mteule wa Mexico, Claudia Sheinbaum.
Rais mteule wa Mexico, Claudia Sheinbaum.Picha: Gerardo Vieyra/NurPhoto/IMAGO

Madrid imesema kitendo cha kutengwa kwa mfalme wake huyo kwenye sherehe hizo za Oktoba Mosi hakikubaliki.

Taarifa iliyotolewa siku ya Jumanne (Septemba 24) na wizara ya mambo ya kigeni ya Uhispania imesema kuwa kutokana na sababu hiyo, serikali imeamua kutokushiriki kwenye sherehe hizo kwa kiwango chochote kile.

Soma zaidi: Mexico yasimamisha uhusiano na balozi za Marekani na Canada

Mexico ilichapisha orodha ya wageni waalikwa wiki iliyopita kwa ajili ya kuapishwa kwa Sheinbaum, ambaye atakuwa rais wa kwanza mwanamke wa taifa hilo la Amerika ya Kusini, kufuatia ushindi mkubwa wa chama chake cha mrengo wa kushoto kwenye uchaguzi wa mwezi Juni.

Ingawa Mexico na Uhispania ina mafungamano ya kihistoria na kiuchumi, lakini mahusiano kati ya taifa hilo la Amerika Kusini na mkoloni wake huyo wa zamani yamekuwa mabaya tangu rais wa Mexico anayemaliza muda wake, Andres Obrador, kuingia madarakani mwaka 2018. Madrid imekataa matakwa yake ya kuomba radhi kwa matukio ya uvamizi na ukoloni wa Uhispania karne tano zilizopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW